Habari za wakati huu ndugu mpenzi msomaji wa makala za mtandao huu, mtandao ambao umelenga kukupatia maarifa ambayo ukiyatumia huta kaa ujute kwanini uliamua kujiunga na mtandao huu ili uwe unasoma makala zake. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri sana katika mapambano nami nasema mapambano yanaendelea na yataendelea.
Wakati unaendelea kupambana nataka nikusihi juu ya jambo moja ambalo unaweza kuwa unalifikiria alafu ukawa unajipotezea muda na hatimaye kujikuta haupati lolote yaani haufanikiwi badala yake unabaki pale pale au unazidi kudidimia chini na hatimaye unajikuta kuwa hu masikini mkubwa sana. Jambo lenyewe ni kule kuweka imani kuwa mafanikio ni bahati. Kama unafikiri kuwa mafanikio ni bahati pole sana maana unajidanganya na unapoteza muda wako. Kama unafanya jambo fulani na unajisemea mwenyewe kuwa nikibahatisha hili jambo ntakuwa mwenye mafanikio ni afadhari uendelee kukaa na kutazama tv tu usifanye chochote maana unapoteza muda wako na nguvu zako pia kwa jambo ambalo halina msingi wala maana yoyote ile bali ujipotoshaji. Hakuna bahati wala bahatinasibu katika mafanikio ndugu msomaji wa makala hii weka hilo katika akili yako.
Kuna watu ambao huwachukulia watu wenye mafanikio kama watu wenye bahati sana, watu hawa ni wale ambao kutokana na imani zao au mitazamo yao huona kuwa mungu anaupendeleo. Kama huwa unasema kuwa fulani ana bahati sana basi wewe unachomaanisha ni kuwa mungu anaupendeleo maana yake ni kuwa kampendelea yule mwenye unamwona kuwa anamafanikio ambayo wewe unayaita bahati na kakubagua wewe ambae hauna kitu hivyo unajiona kuwa hauna bahati. Nami naomba nikuambie tu tena kwa kifupi kuwa mungu hana upendeleo zunguka kote tafuta, uliza na fanya lolote ukipata jibu kuwa mungu anaupendeleo basi jua unapata majibu haya kutoka kwa watu kama wewe na watu kama wewe ni hatari sana katika maisha ya sasa.
Nakuona wewe mfanyakazi uliyekaa ofisini miaka zaidi ya ishirini na tano bado upo katika kitengo kile kile, wakija wenzio wanapandishwa tu vyeo wanakuacha hata wale walio ajiriwa miaka ishirini kabla yako wameshapandishwa vyeo sasa lakini wewe uko pale pale alafu ukikaa na watu hata huogopi unasema dah wenzangu wana bahati sana yaani wao wanapandishwa vyeo tu. Ndugu yangu wewe bahati ni nini?, hebu chunguza kati yao na wewe chunguza kwa umakini utendaji kazi wao na wako je munaendana?, nakuona unapata kigugumizi kujibu kwa kuwa unajijua kuwa wanakuzidi ki utendaji kazi, sasa kama wanakuzidi unataka wewe usiye mtendaji mzuri ndiye upandishwe cheo?. Acha kufanya kazi kwa mazoea eti kisa unauzoefu na kazi hiyo jifunze mbinu mpya za kufanya kazi husika acha habari zako za kusema wana bahati.
Nakuona wewe mfanyabiashara unayefanya biashara ile ile toka mwaka 2000 hadi leo lakini haujasonga mbele biashara ni ile ile na kipato ni kile kile. Wanakuja mwenzio kuanzisha biashara kama yako, bidhaa moja nawe lakini wanauza kukuzidi kila siku, unaanza kusema oooh wanabahati sana hawa watu/ anabahati sana ya wateja nyota yake nzuri. Wewe unakauli mbovu kwa wateja, hujui kuipangilia biashara yako, unawapunja wateja katika vipimo vya bidhaa zako, hautaki kurudisha cheji kwa wateja kwa wakati unajisemea kirahisi rahisi tu njoo baadae ufuate chenji yako au sina chenji kaka yangu au dada, alafu unategemea mteja arudi tena, kwani uko peke yako au huyo mteja hana pengine pa kwenda?, kwa taarifa yako kwa sasa hakuna mteja anayependa mfanyabiashara mbabaishaji ambaye muda mwingine haeleweki. Sasa wewe mwenyewe unafanya biashara kiajabu ajabu wenzio wanasimamia biashara zao vyema alafu unasema wanabahati acha habari zako hizo.
Mafanikio hayahusiani na bahati. Na kama mafanikio yanahusiana na bahati basi kila mmoja wetu ana uhakika wa asilimia mia moja za kubahatika sasa kama wote tuna asilimia zote sawa kwanini wewe hujafanikiwa jiulize na ujijibu sasa.